Alhamisi 14 Mei 2026 - 11:15
Jumuiya ya “Warithi wa Ardhi” katika kulienzi taifa la wapambanaji wa Yemen yafanya kongamano mjini Mashhad Iran

Hawza/ Jumuiya ya “Warithi wa Ardhi” katika kulienzi taifa la wapambanaji wa Yemen imefanya kongamano jioni ya tarehe 10 May kwa ushiriki wa makundi mbalimbali ya wananchi katika uwanja wa Shariati mjini Mashhad Iran.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Mashhad, Jumuiya ya “Warithi wa Ardhi” katika kuenzi taifa la wapambanaji wa Yemen ilifanya kongamano hilo jioni ya tarehe 10 May, sambamba na usiku maalumu wa ziara ya Imam Reza (as), kwa ushiriki wa makundi mbalimbali ya wananchi katika uwanja wa Shariati mjini Mashhad Iran.

Katika kongamano hilo wa wananchi, washiriki wakiwa wamebeba bendera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hizbullah ya Lebanon na Yemen, pamoja na kupaza kauli mbiu mbalimbali, walitangaza mshikamano wao na taifa la Yemen pamoja na mhimili wa muqawama.

Wananchi waliohudhuria hafla hiyo, kupitia kauli mbiu za kuunga mkono mataifa yanayodhulumiwa katika eneo hili yakiwemo Yemen, Palestina, Lebanon na Iraq, walisisitiza umuhimu wa umoja wa mataifa ya Kiislamu mbele ya dhulma na ubeberu wa dunia.

Katika mkondo wa programu hiyo, zilipazwa kauli mbiu mbalimbali za kuliunga mkono taifa la Yemen na vikosi vya muqawama, huku waliohudhuria wakitangaza uungaji mkono wao kwa wapambanaji wa Yemen na kuwataja kuwa ni alama ya kusimama imara mbele ya maadui. Pia walisisitiza mshikamano wa wananchi wa Iran na mataifa ya muqawama ya eneo hili pamoja na kuendelea kuwaunga mkono.

Katika kongamano hilo, ilisisitizwa nafasi ya vikosi vya Ansar Allah vya Yemen katika mabadiliko ya eneo hili, na wakapongeza muqawama na uthabiti wao mbele ya mashinikizo ya kijeshi na kiuchumi ya maadui, huku wakitaja muqawama huo kuwa ni sababu ya kubadilika kwa mlinganyo wa kikanda. Pia walirejelea baadhi ya matukio yanayohusiana na bahari nyekundu na wakasema hatua za vikosi vya Yemen ni ishara ya nguvu na irada ya mataifa ya eneo hili katika kukabiliana na maadui.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha